Koti Jekundu

Little Red Ridinghood - a Swahili version

Hape zamani palikwa na msichana mmoja. Kila mara alivaa koti lake jekundu. Kwa hiyo, watu wote walimwita, "Koti Jekundu".

Siku moja mama yake alimpa kikapu akamwambia, "Bibi yako yu mgonjwa kidogo. Nenda kwake mpelekee chakula hiki kizuri. Shika njia, usitembee msituni, usiseme na wageni."

Koti Jekundu akachukua kikapu kile, akaenda zake.

Wakati anakwenda, aliona maua mazuri sana msituni.  Aliacha njia akaingia msituni kuchuma maua yale.

Mbwa Mwitu alimwona Koti Jekundu. Akamkariba akasema, "Ninachuma maua kwa bibi yangu. Pia nampelekea chakula hiki kumburudisha".

Mbwa Mwitu akaemea, "Ah! Vizuri. Na bibi yako hukaa wapi?"

Koti Jekundu alionyesha mkono wake akasema, "Huko huko, karibu na njia".

Koti Jekundu akasema, "Kwa heri". Akaendelea kuchuma maua.

Mbwa Mwitu akasema, "Haya, kwa heri sasa".

Mbwa Mwitu hakukawia bali alikimbia upesi mpaka nyumbani kwa bibi!

Alipofika mlangoni akapiga, "Hodi!"

Bibi akasema, "U nani?" Mbwa Mwitu kwa sauti tamu akasema, "Ndimi, Koti Jekundu".

Bibi akasema, "Karibu mwanangu!"

Kumbe! Mbwa Mwitu akafungua mlangu, akamrukia bibi, akambia kabisa!

Tena akavalia kitambaa kimoja cha bibi na mwani yake. Akajitia kitandani mwake na akavuta shuka mpaka kidevuni.

Akangoja tu.

Baadaye kidogo, Koti Jekundu akafika mlangoni akapiga, "Hodi!"

Mbwa Mwitu akasema kwa sauti ndogo, "Karibu, mwnanangu".

Koti Jekundu akaingia ndani, akamtazama bibi yake, akashangaa.

Koti Jekundu akasema, "Bibi, macho yako ni makubwa sana!"

Mbwa Mwitu akasema, "Yananifaa kukuona wewe, mwanangu".

Koti Jekundu akasema, "Bibi, pua yako ni kubwa sana!"

Mbwa Mwitu akasema, "Inanifaa kukunusa wewe, mwanangu".

Koti Jekundu akasema, "Masikio yako ni makubwa sana!"

Mbwa Mwitu akasema, "Yananifaa kukusikia wewe, mwanangu".

Koti Jekundu akasema, "Bibi, meno yako ni makubwa sana!"

Mbwa Mwitu akasema, "Yananifaa kukula wewe, mwanangu!"

Mbwa Mwitu akaruka kutoka kitandani ili amle. Looti Jekundu akapiga yowe akalia, "Nisaidie!"

Mkataji miti alimsikia Koti Jekundu, akaja upesi. Akamwua Mbwa Mwitu kwa shoka lake.

Koti Jekundu akasema, "Asante sana!"

Mkataji miti akasema, "Bibi yako yuko wapi?"

Koti Jekundu akasema, "Sijui".

Tena walisikia sauti ndogo inasema, "Mimi hapa tumboni mwake Mbwa Mwitu".

Mkataji alimkata mbwa tumboni na bibi akatoka!

Wote watatu wakafurahi wakala kile chakula kizuri.