Hali Kompyuta na Internet zinaenea Ujapani


| kurudi Orodhani | Mwisho wa Ukurasa | Kampuni za Kijapani | Kutafsiri |

S asa karibu wote wa vijana na watoto Wajapani wamekuwa wanafundishwa kutumia kompyuta katika shuleni. Kompyuta zina wekwa shuleni za msingi (miaka sita) kwa asilimia 100%. Katika shuleni za sekondari (miaka tatu) wanafunzi wanatazamiwa kutumia software kama wordprocecessing, database, painting and drawing na hesabu yenye tables. Wanafunzi wa shuleni za sekondari juu (miaka tatu) au wa vyuo vikuuni (miaka minne) wanafikiriwa kujua sana. Baadhi yao wanafunzi wanaweza kuandika program fulani au kurasa za nyumbani za Internet na kadhalika.

Leo inatazamiwa kuwa kampuni na afisi kubwa zote zina kompyuta. Katika baadhi ya kampuni na afisi, wafanyakazi wanatumia kompyuta sikuzote wakiandika barua, wakihesabia na wakipatia habari. Ni kweli katika kampuni yangu iitwayo "Gakken" afisi nyingi zina kompyuta, hata kompyuta moja kwa mfanyakazi mmojo. Maana yake wafanyakazi wengi wanajua kutumia kompyuta, lakini si wote. Wasiojua au wasiotaka kutumia kompyuta ambao wengi ni wazee wanafanya kazi kama walivyofanya kwa muda mrefu. Vijana wafanyakazi ni lazima wajue mafunzo ya mawasiliano na kutumia kompyuta na mashine ya kisasa.

Katika nyumbani Wajapani asilimia 35% au 40% kuna kompyuta. Idadi ya kompyuta zaidi ya milioni mbili zinauzwa kila mwaka huku. Kwa hivyo kuna mamilioni ya watumiaji wa kompyuta na wasafiri wa Internet katika Ujapani. Kuna Internet providers nyingi sana pia hapa, labda zaidi ya elfu mbili.


Kampuni za kompyuta za Kijapani

K atika Ujapani kuna kampuni nyingi za elektroniki na kompyuta. Kampuni hizo zinafanya biashara ulimwenguni na kupeleka mashine za mawasiliano nyingi kwenda nchini nje. Nitakujulisha baadhi ya kampuni.
NEC
NEC ni kampuni kubwa kabisa zinazotengeneza mashine za elektroniki na kompyuta katika Ujapani. Imetoa PC-98 NX iliyo ni kompyuta mpya kuelekea matumaini ya PC-98 iliyotokeza na Microsoft.
Fujitsuu
Fujitsuu sasa inaendeleza idadi ya nambari mbili kutengenezea mashine za kompyuta. Inajulikana ulimwenguni aina ya kampuni zinazounda kompyuta juu (super computer) zinaenda upesi kabisa.
Panasonic Matsushita
Matsushita inaendeleza kuzidisha sehemu ya kutengenezea kompyuta. Lakini siyo sana kulingana na sehemu nyingine za elektroniki katika kampuni hiyo. Inajulika imetengeneza PD (Photo Disk) kwa mara ya kwanza.
Toushiba
Toushiba inajulikana ni kampuni muhimu kutengeneza kompyuta dogo. Kompyuta za 'laptop' au 'noteboook' zimeundwa na Toushiba kwa idadi kubwa sana ulimwenguni.

Programu ya kutafsiri

W ajapani wengi hawajui lugha za kigeni. Ingawa wamefundishwa Kiingereza shuleni ya sekondari, ya sekondari juu na chuoni kikuu, hawawezi kusema na kuandika vizuri. Kwa sababu hakuna nafasi ya kutumia lugha za kigeni hata Kiingereza nchini hii, wanatumia Kijapani tu mara zote wakifanya kazi, mafunzo na mambo yoyote. Kama wakijilazimisha kuambia mgeni kutoka nchi nje, wataelekea kumfanyiza mtafsiri kueleza maana ya mazungumzo wao. Katika kurasa za Internet Wajapani wanaweza kutumia programu ya kutafsiri. Kuna programu nyingi ya kutafsiri kutoka Kiingereza, Kikorea n.k. kwenda Kijapani, na kutoka Kijapani kwenda lugha nyingine. Kwa hivyo baadhi ya Wajapani wanasema kwamba haifai kujaribu kujifunza lugha za kigeni. Kama kompyuta zitaweza kufanya kazi ya kutafsiri, hakuna lazimu kujifunza lugha za kigeni shuleni, sivyo? Lakini wasemaji na wakurugenzi ya elimu na lugha za kigeni hawakubaliani navyo.

Baadhi ya programu ya kutafsiri kutoka Kiingereza hadi Kijapani zinapatikana kutoka ukurasani wa Internet. Unaweza kutazama orodha ya kampuni zinazoeleza programu hizo ukurasani wangu. Angalia "Entertainment" katika "Links" ya Toptown. Unaweza kujaribu kutumia mmoja au mbili. Kabla ya kujaribu lazima kupata herufi za Kijapani. Yapatikana katika Microsoft Internet Explorer Multi Language Support for Windows95 &NT ukisoma andishi la Kijapani.


| kurudi Orodhani | Mwisho wa Ukurasa | Kampuni za Kijapani | Kutafsiri |

Kuniandikia barua ya Email: kwa NH
Ilitengenezwa na NH, Kawasaki 1997. Asante.